Dkt. Abbasi atoa maelekezo kuinua sanaa nchini

0
306

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi, leo Novemba 30, 2020 ameanza ziara ya kukutana na wadau wa sanaa kwa kukutana na wakuu wa taasisi zilizo chini ya wizara hiyo zinazoratibu masuala ya sanaa nchini.

Dkt. Abbasi ameelekeza taasisi hizo kuwa kiungo kati ya wadau wa sanaa na serikali na amezitaka ziwe karibu na wadau hao, ziwahudumie kwa karibu na zaidi zibuni mambo mapya ya kuishauri serikali katika kutekeleza azma ya kuiinua sekta ya sanaa.

“Serikali imeahidi kuinua sekta ya sanaa na dhamira kubwa ipo, ni juu yenu kushirikisha wadau ili kupata mrejesho utakaoelezea sekta inataka kufanyiwa nini na Serikali ili ikue,” amesisitiza Dkt. Abbasi.