Dkt Abbas kuendelea kuwa Msemaji Mkuu wa Serikali

0
308

Rais Dkt. John Magufuli amesema kuwa, Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Hassan Abbas ataendelea kuwa Msemaji Mkuu wa Serikali.

Rais Magufuli ameyasema hayo Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuwaapisha Viongozi mbalimbali aliowateua hivi karibuni.

Amesema kuwa kabla ya uteuzi wa sasa, alipokuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt Abbasi amefanya kazi nzuri katika kuisemea Serikali.

Rais Magufuli ameongeza kuwa, ingewezekana kumuacha katika nafasi hiyo ya awali kwa utendaji wake mzuri, lakini imebidi aondolewe kwa sababu wakati wa kupandishwa ngazi ya juu umefika.