Dirisha la udahili awamu ya pili lafunguliwa

0
103

Tume ya vyuo vikuu Tanzania (TCU) imefungua dirisha la awamu ya pili ya udahili wa wanafunzi wa Elimu ya Vyuo vya elimu ya juu nchini kwa awamu ya pili ngazi ya Shahada ya kwanza kwa mwaka wa masomo 2022/2023 ambapo majina ya waliodahiliwa katika awamu hiyo watatangazwa na vyuo husika.

Awamu ya pili ya udahili itadumu kwa wiki mbili nakufungwa Septemba 06, 2022.

Aidha kwa awamu ya kwanza jumla ya waombaji 75,163 sawa na asilimia 70.71 wamepata nafasi vyuoni.