Diallo ateuliwa mwenyekiti TFRA

0
215

Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi ambapo amemteua Antony Diallo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA).

Diallo anachukua nafasi ya Profesa Anthony Mshandete ambaye amemaliza muda wake.

Uteuzi huo umeanza Februari 09, 2023.

Pia Dkt. Samia amemteua Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali George Waitara kwa kipindi kingine kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA).

Uteuzi huo umeanza Februari 13, 2023.