Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Nchini (DCEA) imekamata kilo 900 za dawa za kulevya katika kipindi cha miezi mitatu.
Kamishna Jenerali wa DCEA Gerald Kusaya amesema, rekodi hiyo ya kukamata kiasi hicho cha dawa za kulevya haijawahi kufikiwa nchini.
Kusaya ametoa takwimu hizo mkoani Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya kutembelea ofisi za TBC, ziara iliyokuwa na lengo la kujionea namna Idara mbalimbali za shirika hilo zinavyotekeleza majukumu yake.
Pia ametoa rai kwa vyombo vya habari nchini kushirikiana na DCEA katika mapambano.dhidi ya dawa za kulevya.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TBC Dkt. Ayub Rioba Chacha amesema TBC itaendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu mapambano dhidi ya dawa za kulevya.