Dawa za binadamu zatupwa Katavi

0
300

Dawa za binadamu ambazo hazijaisha muda wake wa matumizi, zimekutwa zimetupwa mjini Mpanda mkoani Katavi.

Dawa hizo ambazo nyingi ni mali ya Serikali zina nembo ya Bohari ya Dawa (MSD) na zimekutwa zimetupwa katika eneo la daraja la Kigamboni.

Wataalam wa afya wilayani Mpanda wanaendelea kufanya tathmini, ili kujua thamani halisi ya dawa hizo.