Darasa la nne waanza mitihani

0
194

Watahiniwa milioni.1.71 wa darasa la nne kutoka katika shule za msingi 18,654 za Tanzania Bara, leo wameanza mitihani yao ya upimaji wa kitaifa (SFNA) inayofanyika ka muda wa siku mbili.

Watahiniwa hao wavulana ni 846,380 ambao ni sawa na asilimia 49.32, wasichana ni 869,677 sawa na asilimia 50.68 na watahiniwa wenye mahitaji maalum ni 5,468.

Kwa mujibu wa Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), ikilinganishwa na mwaka 2021 mwaka huu kuna ongezeko la watahiniwa wa darasa la nne kwa asilimia 2.04.