DARAJA LA MKAPA LILIVYOFUNGUA UCHUMI WA KUSINI MWA TANZANIA

0
208

Daraja la Mkapa lililopo Ikwiriri, Kusini mwa Tanzania katika Mto Rufiji ndilo daraja refu zaidi nchini Tanzania likiwa na urefu wa mita 970.

Daraja hilo lililopewa jina la Rais Mstaafu, Marehemu Benjamin Mkapa lilizinduliwa mwaka Agosti 2, 2003 wakati akiwa madarakani baada ya kukamilika kwa ujenzi uliogharimu dola za kimarekani milioni 30 (shilingi bilioni 69).

Kabla ya ujenzi wa daraja hilo, wananchi walilazimika kutumia kivuko kutoka upande mmoja kwenda mwingine, hali iliyokuwa na changamoto nyingi pale muda wa kazi kuisha au kivuko kuharibika.

Daraja hilo limefungua uchumi wa ukanda wa kusini kwa kurahisisha shughuli za usafiri, usafirishaji na uwezo wa watu kutoka upande mmoja kwenda mwingine.