Dar yachangia 70% ya kodi nchini

0
153

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaaam Amos Makalla amesema jiji la Dar es Salaam limevunja rekodi ya kuchangia asilimia 70 ya kodi katika kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka wa fedha 2022/2023.

Kwa mujibu wa ripoti ya Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) imekusanya Sh12.4 trilioni katika kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka wa fedha 2022/23 yaani Julai hadi Desemba 2022. Makusanyo hayo ni sawa na asilimia 99 ya lengo la makusanyo ya Sh12.48 trilioni.