Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, – Paul Makonda amewataka wakazi wa mkoa huo kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuimarisha uchumi wa familia zao na Taifa.
Makonda ametoa kauli hiyo mara baada ya kukagua mradi wa ujenzi wa kituo kikuu cha mabasi unaoendelea katika eneo la Mbezi jijini Dar es salaam.
Amewataka wakazi hao wa mkoa wa Dar es salaam kutumia fursa ya kuwepo kwa ujenzi wa mradi huo kufanya shughuli mbalimbali zitakazowaongezea kipato.
Kwa sasa ujenzi wa mradi wa kituo kikuu cha mabasi unaoendelea katika eneo la Mbezi umefikia asilimia sabini na kwamba utakapokamilika kituo hicho kitakua na uwezo wa kuhuhudumia mabasi mia saba na magari madogo 280 kwa siku.