Daladala zasitisha huduma

0
225

Madereva wa mabasi madogo ya kubeba abiria maarufu kama daladala mjini Njombe, wamesitisha kutoa huduma ya usafiri kwa muda usiojulikana.

Madereva hao wa daladala wamefikia hatua hiyo ili kushinikiza mamlaka husika kusimamia biashara ya usafiri wa vyombo vya moto na kusikiliza madai yao.

Wakizungumza na Mwandishi wa TBC mkoani Njombe, baadhi ya madereva hao wamesema wamechoshwa na vitendo vinavyofanywa na madereva bajaji vya kufanya biashara ya kupakia abiria  nje  ya maeneo waliyopangiwa na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), na hivyo kuvuruga safari za daladala.

Madereva hao pia wameilaumu LATRA kwa kushindwa kudhibiti jambo hilo ambalo linaathiri biashara yao kwa kuwa wamekuwa wakipoteza muda wa kufanya kazi kwa kugombania abiria.