Dagaa ni zao la kimkakati Ulega

0
191

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wanatengeneza miundombinu mizuri na kuwapatia Wavuvi wanaoishi kandokando ya ukanda wa Ziwa Tanganyika na maeneo mengine vifaa vya kisasa vya uvuvi ili viwasaidie kuongeza thamani ya zao la Dagaa na kupunguza upotevu wa zao hilo baada ya kuwavua.

Ulega aliyasema hayo wakati wa ziara yake aliyoifanya katika vijiji vya Buhingu na Katumbi vilivyopo wilayani Uvinza, Mkoani Kigoma hivi karibuni.

Akiongea na Wavuvi wa vijiji hivyo kwa nyakati tofauti Ulega amesema Serikali imedhamiria kukuza uchumi wa buluu na ndio maana inatengeneza miundo mbinu mizuri ya kuchakata dagaa na mazao mengine ya samaki ili kuwaongezea thamani na waweze kuuzika kwa bei nzuri na wananchi wafaidike na zao hilo.