Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo amekemea tabia ya baadhi ya wazazi na walezi wilayani Morogoro kuwatumia watoto wa kike kama kitega uchumi kwa kuwaozesha wakiwa na umri wa kwenda shule.
Chongolo amesema hayo mara baada ya kuwasili wilayani Morogoro akitokea wilayani Ulanga, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya siku 9 mkoani Morogoro yenye lengo la kukagua uhai wa chama katika wilaya zote za mkoa huo.
Amesema baadhi ya wazazi na walezi wamekuwa wakiwatumia watoto wa kike kama njia ya kujipatia fedha, na kuwakosesha haki yao ya kupata elimu ambayo inatolewa na serikali bila malipo.
Awali Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Sophia Mjema alisema CCM itaendelea kujiimarisha kuanzia ngazi zote za chini hadi Taifa na kuwataka wanachama wa chama hicho kuendelea kuwa wamoja.