Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo amewapogeza Jumuiya ya umoja wa wanawake Tanzania (UWT) kwa kazi kubwa wanayoendelea kuifanya katika maeneo mbalimbali nchini ikiwa ni pamoja na kuandikisha wanachama wapya, kuhimiza wanachama kulipa ada na kubuni miradi mbalimbali ya kiuchumi.
Katibu Mkuu ametoa pongezi hizo akiwa mgeni rasmi katika kikao cha kawaida cha Baraza Kuu la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) lililofanyika leo tarehe 20 Disemba, 2021 Makao Makuu ya Chama jijini Dodoma.
Chongolo ameeleza kuwa, Maeneo hayo matatu kwa CCM ni muhimu kwani bila kuyawekea mkazo hakuna Chama wala Jumuiya imara.
Aidha, UWT kupitia kwa Mwenyekiti wake Taifa Gaudentia Kabaka, imetoa tamko la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuunda kamati maalum ya kumshauri kuhusu masuala ya usawa wa kijinsia, ambapo itasaidia katika kufikia malengo ya hamsini kwa hamsini katika fursa mbalimbali.
Kikao hicho cha kawaida, kimehudhuriwa pia na baadhi ya Wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa akiwemo Katibu wa NEC, Oganaizesheni Maudline Castico na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Dkt. Edmund Mndolw