Chongolo awahamasisha wanasiasa kusoma shule ya Uongozi

0
116

Katibu Mkuu Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo amewahimiza viongozi na wanasiasa wa vyama vyote kujiunga na chuo cha elimu ya Uongozi Kibaha mkoani Pwani ili kuwajengea uwezo wa kuwa washindani na wabobezi wa masuala ya Uongozi Katika ngazi mbalimbali.

Chongolo amesema hayo wakati wa ufunguzi wa shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere Kibaha mkoani Pwani na kutangaza nafasi kwa kila anayehutaji kupata elimu ya Uongozi aende kujiunga katika chuo hicho.

Aidha Chongolo amesema kuwa elimu itakayotolewa chuoni hapo ni mafunzo ya yenye kuendana na kasi ya uchumi, Diplomasia na Teknolojia ya kisasa ambacho kitatoa kozi za muda mfupi, wakati na mrefu ili kuendana na kasi ya wahitaji.

“Chuo hiki kina hadhi ya Kimataifa hivyo niawalike wanasiasa wa vyama vingine Pia kuja kujiunga na chuo hiki ili kuwajenga Katika Uongozi utakaowasaidia kwenye nafasi zao za Uongozi.”-ameongeza Katibu Mkuu Chongolo.

Akihutubia kwenye ufunguzi huo Chongolo amesema masomo yatakayotolewa yataisadia kujenga vijana na viongozi watakuaokuwa nanuwezo wa kuwa na uelewa mkubwa wa masuala ya Uongozi na kujitawala.

Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere imejengwa kwa ushirikiano wa Chama cha (CPC) China (CCM) Tanzania, (ANC) Afrika Kusini, (FRELIMO) Msumbiji, (SWAPO) Namibia, (ZANU-PF) Zimbabwe na (MPLA) Angola.