Chongolo atoa agizo TANROADS

0
165

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo ameuagiza Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), kukamilisha ujenzi wa kiwango cha lami barabara inayounganisha wilaya za Malinyi mkoani Morogoro na Namtumbo mkoani Ruvuma ili iweze kupitika mwaka mzima.

Chongolo ametoa agizo hilo alipokuwa akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa wilaya ya Malinyi ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku 9 mkoani Morogoro yenye lengo la kukagua uhai wa chama na kutembelea mashina.

Awali akizungumza na wakazi wa kijiji cha Itete akiwa njiani kutoka wilayani Kilombero kuelekea Malinyi, Chongolo alisema CCM haitawavumilia wenyeviti wa vijiji na vitongoji watakaokuwa sehemu ya kuchochea migogoro baina ya wakulima na wafugaji nchini.