Chongolo ataka kukamilika ujenzi wa zahanati Kinambeu

0
151

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo, amekwamua ujenzi wa zahanati ya Kinambeu iliyopo Iramba mkoani Singida, uliokwama kwa zaidi ya miaka 10.

Chongolo amekwamua ujenzi huo kwa kuielekeza Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuhakikisha inapeleka fedha haraka ili ujenzi huo ukamilike na kuwaondolea adha wananchi ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya.

Chongolo ametoa maelekezo hayo alipotembelea na kukagua majengo ya zahanati hiyo ya
Kinambeu ambayo ujenzi wake ulianza mwaka 2011.

Hadi sasa ujenzi wa zahanati hiyo umegharimu shilingi milioni 185.9.