Chongolo ashtushwa majengo kutelekezwa

0
198

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo ametoa muda wa siku 14 kwa Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Angellah Kairuki kufika katika kituo cha afya Mikese kilichopo wilayani Morogoro ili kujua chanzo cha kutelekezwa kwa majengo ya huduma ya mama na mtoto kwa zaidi ya miaka mitatu.

Chongolo ametoa muda huo baada ya kuwasili katika kituo hicho cha afya ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku tisa mkoani Morogoro.

Amesisitiza kuwa haiwezekani kuona serikali imewekeza zaidi ya shilingi milioni 400 katika ujenzi wa miundombinu hiyo ya afya, lakini bado hakuna tija kwa wananchi.

Baadhi ya wakazi wa eneo hilo wamesema kukamilika kwa kituo hicho cha afya Mikese kutawapunguzia adha akina mama wajawazito ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma za mama na mtoto nje ya eneo hilo la Mikese.