Chongolo: Acheni tabia za kuuza ardhi hovyo

0
218

Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Daniel Chongolo amewataka wanachama wa chama hicho kuacha tabia ya kuuza ardhi kwenye maeneo yao.

Chongolo ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wanachama wa Chanika wilayani Handeni mkoani Tanga. Amesema suala la uuzaji wa ardhi kiholela limesababisha kuwepo kwa migogoro jambo linalochangia kuchelewa kwa maendeleo.

“Nawaomba sana wanachama msiuze ardhi kwani ardhi ni rasilimali muhimu tulioirithi kutoka kwenye vizazi vyetu,hivyo haifai kabisa kuuza na badala yake tuitunze,”- Amesema Chongolo.

Aidha amesema mahali popote panapokua na migogoro ya ardhi shughuli za maendeleo zinachelewa hali inayopelekea kuzorota kwa uchumi.

Na, Bertha Mwambela Tanga