Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo, amewasili wilayani Gairo mkoani Morogoro kuanza ziara ya siku tisa ambayo ataifanya katika mkoa huo.
Akiwa wilayani humo, Chongolo atakagua shughuli za chama na kuzungumza na watendaji mbalimbali pamoja na wananchi.