Chifu wa ukoo wa Mkapa akimuelezea Rais Mstaafu Benjamin Mkapa

0
203

Chifu Mkonona wa Ukoo wa Mkapa amesema familia imepokea kwa huzuni kubwa taarifa za kifo cha mwanao na ndugu yao Benjamin Mkapa kwani bado walimuhitaji.

Akizungumza na Shirika la Utangazaji Tanzania, Chifu amesema kuwa Marehemu Benjamin Mkapa aliwapa heshima kubwa serikalini na hata kwenye jamii, lakini hajua kama heshima hiyo itaendelea kuwepo baada ya mpendwa wao kufariki.

Ameongeza pia kiongozi huyo alikuwa chachu ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika eneo la Lupaso kama vile kuhakikisha upatikanaji wa maji, umeme pamoja na barabara.

Hata hivyo amewashukuru waombolezaji wote waliofika kuwajulia hali, kuwapo pole pamoja na kutoaa misaada ya hali na mali, kwani kupitia huduma hizo wanapata faraja na kujiona hawapo peke yao.