Chifu Hangaya atembelea makumbusho ya Bujora

0
130

Rais Samia Suluhu Hassan (Chifu Hangaya) ametembelea makumbusho ya Bujora mkoani Mwanza ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake mkoani humo.

Akiwa katika Makumbusho hayo, Rais Samia ametembezwa katika eneo la utalii kwa mila, tamaduni na desturi za Wasukuma, amejionea nyumba za sili za kabila hilo pamoja na nyumba ya Mtemi.

Aidha, Rais Samia aliketi katika kiti cha Mtemi, alichokalia wakati anaapishwa.