Cheche za Wabunge kuhusu kupanda kwa bei ya mafuta

0
943

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo limelazimika kusitisha shughuli zake ili kuwaruhusu Wabunge kujadili hoja ya dharura kuhusu suala la kupanda kwa bei ya mafuta, jambo lililosababbisha kupanda kwa bei za bidhaa mbalimbali nchini.

Hoja hiyo imewasilishwa bungeni jijini Dodoma na Mbunge wa jimbo la Kilindi mkoani Tanga Omari Kigua.

Akiwasilisha hoja hiyo, Kigua aliliomba Bunge kusitisha shughuli zake kwa muda na kujadili suala hilo la kupanda kwa bei ya mafuta ambalo ni jambo muhimu kwa maslahi ya Taifa.

https://www.youtube.com/watch?v=hbX96TClta0

Baadhi ya Wabunge waliopata nafasi ya kuchangia hoja hiyo wamesema bei za mafuta zimepanda kwa kasi, jambo ambalo limeleta adha kubwa kwa wananchi hasa wa kipato cha chini na hivyo kuitaka Serikali kufanya jambo la dharura kunusuru hali hiyo.

Wengine wameitaka Serikali kulichukulia kwa uzito suala hilo, ili hali irejee kama kawaida