Chatu aliyeonekana Chato, apelekwa kwenye pori Kahama

0
180

Nyoka aina ya Chatu aliyeonekana kwenye kata ya Makurigusi wilayani Chato mkoani Geita, amechukuliwa na kupelekwa katika pori la akiba la Kigosi lililopo wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Kufuatia tukio hilo, Afisa Wanyamapori kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), – Laurent Yohana ametoa rai kwa Watanzania wote wanapoona Wanyama ambao wanaweza kuhatarisha maisha yao, watoe taarifa kwenye mamlaka husika kabla Wanyama hao hawajaleta madhara.