Chatanda : Tuziangalie taasisi zinazoharibu maadili

0
177

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa Mary Chatanda amewataka viongozi wa ngazi mbalimbali nchini kuziangalia taasisi zikiwemo shule na nyingine zisizo za Kiserikali ambazo zinahamasisha na kufundisha maadili na utamaduni usio wa Kitanzania.

“Zipo taasisi zisizo za kiserikali (NGO) ambazo zipo kwenye mikoa yetu, zipo nchini hapa, ndio hao wanaojiita wafadhili. Huko ndiko wanakopitisha fedha za mambo machafu haya… Niwaombe viongozi wa serikali, wakuu wa wilaya, wakurugenzi tuziangalie hizi NGO tulizonazo huku, tuzifanyie kazi, tuzijue, fedha zao zinaingia kwa njia gani, zina shughuli gani?. Wengine wameanzisha shule na huko ndiko wanakokwenda kuwafundisha wale watoto wadogo”. Amesema Chatanda

Ameyasema hayo wakati wa mkutano wa hadhara mkoani Njombe ikiwa ni sehemu ya ziara ya viongozi wa ngazi ya juu wa UWT mkoani humo, ziara iliyokuwa na lengo la kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM kwenye mkoa huo.