Chanjo kusaidia kupunguza maambukizi

UVIKO - 19

0
150

Mkuu wa mkoa wa Iringa Queen Sendiga ameongoza wakazi wa mkoa huo kupata chanjo ya UVIKO – 19 huku akiwaondoa hofu kwamba wakipata chanjo maambukizi yatapungua.

Hata hivyo Sendiga amewataka wana Iringa kuendelea kuchukua tahadhari na kuvaa barakoa kwenye maeneo ya msongamano.

TBC imeshuhudia watumishi wa afya wakipokea chanjo hiyo wa mwanzo na wazee wakipewa kipaumbele.

Vituo 15 vya kutolea chanjo vimeandaliwa kwa ajili ya zoezi hilo.