Rais Samia Suluhu Hassan na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya wamekubaliana kuendelea kushughulikia changamoto mbalimbali ambazo Wafayabiashara wa Tanzania na Kenya wamekuwa wakikutana nazo.
Amesema miongoni mwa changamoto kubwa kwa Wafanyabiasara hao ni ile ya vikwazo visivyo vya kodi katika maeneo ya mpakani, ambayo imekuwa ni kero ya muda mrefu kwa Wafanyabiashara hao.
Rais Samia Suluhu Hassan anayeendelea na ziara yake ya kikazi ya siku mbili nchini Kenya ametoa kauli hiyo wakati wa mkutano na Waandishi wa habari jijini Nairobi, mara baada ya mazungumzo yake ya faragha na Rais Uhuru Kenyatta wa nchi hiyo.
Amesema wameiagiza Tume ya ushirikiano baina ya Tanzania na Kenya kuandaa utaratibu wa kukutana mara kwa mara, kwa lengo la kujadili namna ya kutafuta suluhu ya vikwazo vya kibishara vinavyojitokeza katika maeneo ya mpakani.
Rais Samia Suluhu Hassan na Rais Kenyatta wamewaelekeza Mawaziri wa afya wa Tanzania na Kenya kukutana na kupanga utaratibu unaofaa kwa Wafanyabiashara kufanyiwa vipimo vya corona kwa haraka, ili waweze kupata majibu na kuendelea na biashara zao.