Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa wito kwa kamati ya uboreshaji na undelezaji wa chaneli mpya utalii ya Tanzania Safari kuweka jitihada za uwekezaji kwa kusambaza huduma ya chaneli hiyo katika visimbusi mbalimbali ili kupanua wigo wa kuonekana ndani na nje ya nchi.
Waziri Mkuu Majaliwa ametoa wito huo Jijini Dodoma wakati akipokea taarifa ya maendeleo ya chaneli hiyo ilipofikia tangu kunzishwa kwake.
Kamati ya uboreshaji na undelezaji wa chaneli hiyo imewasilisha taarifa ya maendeleo .
Waziri Mkuu Majaliwa ameipongeza kamati hiyo na kutoa wito wa kupanua wigo wa chaneli hiyo katika uwekezaji.
Pia ameitaka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo kuingiza bajeti kwa ajili ya Tbc kuweza kuendesha chaneli hiyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tbc Dokta Ayub Rioba amesema kupitia chaneli hiyo watanzania watajua vivutio vilivyopo na kuvutunza .
