Chaneli ya Utalii hadharani

0
1585

Chaneli ya Utalii inayojulikana kama Tanzania Safari inazinduliwa rasmi hii leo jijini Dar es salaam na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Chaneli hiyo ya Utalii imeanzishwa kufuatia wazo lililotolewa na Rais John Magufuli
mwezi Mei mwaka 2017 alipozitembelea ofisi za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC, Mikocheni jijini Dar es salaam.

Akitoa wazo hilo, Rais Magufuli alisema kuwa Chaneli hiyo maalumu ya Utalii itasaidia kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo nchini.

Miongoni mwa wadau waliofanikisha uanzishwaji wa Chaneli hiyo mpya ya Utalii ya Tanzania Safari ni Shirika la Utangazaji Tanzania, Wizara ya Maliasili na Utalii, wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na wizara ya Mifugo na Uvuvi.

Mkurugenzi wa Ufundi wa TBC, -Upendo Mbele amesema kuwa mitambo ya kurushia matangazo ya chaneli hiyo mpya ya utalii ni ya kisasa na ipo tayari kwa ajili ya kuzinduliwa rasmi.