Chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA) kimezindua Opereseheni +255, yenye lengo la kutoa hamasa kwa Wananchi kukiunga mkono chama hicho katika harakati zake mbalimbali.
Operesheni hiyo imezinduliwa mkoani Kigoma na Viongozi mbalimbali wa Kitaifa wa CHADEMA wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho Taifa Freeman Mbowe kwa lengo kujiimarisha kwa kujitathmini maeneo yaliyosababisha wapoteze mvuto kwa wananchi wa maeneo hayo na kufanyia marekesho dosari zilizowarudisha nyuma na kurudisha imani kwa wananchi
Baada ya Opereseheni +255 kuzinduliwa Kigoma, Viongozi hao wa CHADEMA watazunguka kwa muda wa miezi miwili katika mikoa mbalimbali ya Kanda ya Magharibi ambayo ni kigoma yenyewe, Tabora na Katavi kwa lengo kuwaomba Wananchi wakiunge mkono chama hicho katika harakati zake mbalimbali.