Meya wa jiji la Mbeya pamoja na Makamu Meya wa jiji hilo ambao wote wanatoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wametangaza kukihama chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Viongozi hao pamoja na Madiwani 11 wa Mbeya Mjini kutoka chama hicho cha CHADEMA wametangaza uamuzi huo jijini Dodoma na kupokelewa na Katibu Mkuu wa CCM Dkt Bashiru Ally.
Akizungumza mara baada ya kuwapokea viongozi hao, Dkt Bashiru amesema kuwa huo ni ugeni mkubwa kuupokea ndani ya CCM katika siku za hivi karibuni.
Viongozi hao wamesema kuwa, wameamua kujiunga na CCM ili kuunga mkono jitihada za Rais John Magufuli za kuwaletea Watanzania maendeleo.