CHADEMA kutoshiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa

0
190

Chama Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza kujiondoa kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa uliopangwa kufanyika Novemba 24 mwaka huu.

Uamuzi huo umetangazwa hii leo na Mwenyekiti CHADEMA Taifa, – Freeman Mbowe wakati wa kikao cha dharura cha Kamati Kuu ya chama hicho kilichofanyika jijini Dodoma.

Mbowe amesema kuwa, CHADEMA imeamua kujiondoa katika uchaguzi huo, kutokana na kutoridhishwa na baadhi ya mambo katika mchakato nzima wa kuelekea katika uchaguzi huo.