CHADEMA kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa

0
223

Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa Freeman Mbowe amesema kuwa, chama hicho kitashiriki katika uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 24 mwaka huu.

Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Mbowe ametoa wito kwa Wananchi kujitokeza kujiandikisha kwenye Daftari la Orodha ya Wapiga kura ili waweze kushiriki kwenye uchaguzi huo.

Aidha amesema kuwa, kususia uchaguzi huo kutawanyima Wananchi haki yao ya msingi ya kuwachagua Viongozi wao wa Serikali za Mitaa ambao ndio watashiriki kutatua kero mbalimbali.