‘CHA ARUSHA’ UKIINGIA VIBAYA LAZIMA UWE MWENDAWAZIMU

0
140

Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongella ameeleza ni kwa namna gani dawa za kulevya aina ya bangi maarufu ‘cha Arusha’ ni hatari zaidi mkoani humo.

Mongella ameyasema hayo katika maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za kulevya duniani, yaliyofanyika jijini Arusha.

‘’….. Mheshimiwa Rais kwa sasa inasemekana duniani hakuna bangi kali kama ya Arusha, tumeambiwa na Dokta Mfisi, Dokta Mfisi naomba usimame ambaye unaonekana ndio mtaalamu bingwa kwenye mamlaka”. Amesema Mongella na kuongeza kuwa

“Tumeulizia sana kwa miezi hii miwili tunaambiwa hii inayoitwa maarufu kama ‘cha Arusha’ …..hii cha Arusha nasikia mpaka huko wanasema ukiingia vibaya lazima uwe mwendawazimu mara moja”

“Na inasifa kwamba hii ni organic kule inapolimwa Kisimiri ni eneo lenye rutuba sana na tumeamua kwamba kwa dhamana ulizotupa…kampeni ya kushirikishana na jamii kumaliza tatizo hili tumeianza, na Kamishna Jenerali na timu yake wamefanya kazi kubwa sana“. Amesema Mongella