CCM yawasimamisha viongozi wa gazeti la uhuru

0
178

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimewasimamisha kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Uhuru Media, Ernest Sungura, Mhariri Mtendaji, na Msimamizi wa Gazeti, Rashid Zahoro kutokana na kuandika taarifa isiyo sahihi kumhusu Rais Samia Suluhu Hassan.

Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongo ametoa uamuzi huo leo baada ya gazeti hilo kuchapisha habari inayodai kuwa Rais Samia Suluhu Hassan hana mpango wa kugombea urais mwaka 2025.

Mbali na hilo, Chongolo amesimamisha uchapishaji wa gazeti la Uhuru kwa muda wa siku saba