CCM yatoa tamko suala la Bodaboda kuingia mjini

0
231

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo amesema, watu wa bajaji na bodaboda mkoa wa Dar es salaam hawawezi kuondolewa katikati ya jiji hilo.

Chongolo ameyasema hayo, leo tarehe 22 Aprili, 2022 katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Ilala.

Amesema kuwa, hao ni watu muhimu na hawawezi kuachwa kwa sababu wanajitafutia riziki halali, ambapo amewasihi watu waache kutoa taarifa za kupotosha umma kuwa wanaondoshwa mjini.

“Kinachofanyika sio kuwazuia bodaboda na bajaji wasiingie mjini bali ni kuwaratibu ili kuwawekea vituo rasmi vitakavyoweza kutambulisha watu wanahitaji kutumia usafiri huu”, amese Chongolo

Chongolo amesisitiza kuwa waendesha bajaji baadhi yao ni watu wenye ulemavu, ambao ni kundi maalum linalopata mikopo inayotolewa na Halmashauri asilimia 10, hivyo lazima waheshimiwe kwa kuwaweka eneo maalum kwa ajili yao ili wasigombanie abiria na watu wengie wasiokuwa na ulemavu.