CCM yasema haihusiki na kuenguliwa kwa baadhi ya Wagombea

0
191

Chama  Cha Mapinduzi (CCM) kimesema  kuwa Wagombea walioenguliwa katika uchaguzi wa Serikali za Mtaa ni kutokana na kutofuata sheria za uchaguzi huo.

Akizungumza na Waandishi wa habari katika ofisi ndogo za Makao Makuu ya CCM jijini Dar es salaam, Katibu wa Itakadi na Uenezi wa Chama hicho Humphrey Polepole amesema kuwa, CCM haihusiki kwa namna yoyote ile katika kuenguliwa kwa baadhi ya Wagombea katika uchaguzi wa Serikali za Mtaa.

Amesema kuwa CCM iliwekeza katika kutoa elimu kuhusu uchaguzi huo, wakati vyama vingine vilishindwa kufanya hivyo, na badala yake vinaitupia lawama kuwa imefanya hujuma.

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa umepangwa kufanyika Novemba 24 mwaka huu, na tayari baadhi ya Wagombea wameenguliwa kushiriki katika uchaguzi huo kutokana na kutofuata sheria.