CCM yaridhishwa na ujenzi wa gati Tanga

0
150

Kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Tanga imeeleza kuridhishwa na kiwango cha ujenzi wa gati mpya kwenye bandari ya Tanga, yenye urefu wa mita 150 ambayo imejengwa kwa garama ya shilingi bilion 270.

Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tanga Dkt. Henry Shekifu mara baada ya kamati hiyo kutembelea bandari hiyo na kujionea hali halisi ya utekelezaji wa ilani ya chama hicho.

“Tunaishukuru sana serikali kwa hatua hii kubwa kwa sababu kuboreshwa kwa miundombinu hii, kutasaidia kuifungua bandari yetu ambayo sisi tunaona ndiyo kitovu cha uchumi wa mkoa wetu.” amesema Dkt. Shekifu

Amesema kukamilika Kwa ujenzi huo kumesaidia bandari hiyo ya Tanga kupokea meli kubwa za mizigo tofauti na ilivyokua awali ambapo kina cha bandari hiyo kilikua kifupi.