Chama cha mapinduzi CCM, kimeanzisha kituo maalum cha kupokea taarifa za wanachama wake watakaoanza kampeni mapema kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kupitia chama hicho.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho Humphrey Polepole
amesema kituo hicho pia kitatumika kupokea taarifa za kuwabaini wanachama watakaovunja kanuni na maadili ya chama.
Polepole ameongeza kuwa mchakato wa kutafuta wagombea wa nafasi mbalimbali kwa tiketi ya chama hicho utaanza mara baada ya kuvunjwa kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano.