CCM yajivunia mafanikio yake kwa zaidi ya miongo minne

0
139

Katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 45 ya kuanzishw kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) hapo kesho, chama hicho kinajivunia mafanikio makubwa yaliyoweza kufikiwa ndani ya kipindi hicho.

Moja ya mafanikio yaliyofikiwa ni pamoja na kumiliki Uchumi mkubwa ambao unakisaidia Chama hicho kujiendessha na kujisimamia chenyewe.

Akizungumza na vyombo vya habari mjini Musoma, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na uenezi wa chama hicho Shama Hamdu Shaka amesema mpaka sasa chama hicho kinamiliki zaidi ya Trioni 1.5

Shaka amesema kitendo cha CCM hicho kumiliki uchumi huo ni kutokana na kuwa na viongozi bora wenye uwezo wa kusimamia miradi kikamilifu hali inayowafanya wazidi kuimarika kiuchumi.

Amesema katika miaka 45 hii hakuna chama kingine ambacho kimeweza kuvunja rekodi hiyo, hivyo kuwafanya waendelelee kuwa namba moja katika uchumi.