Mgombea Mwenza wa urais kwa tiketi ya CCM, Samia Suluhu Hassan amesema wakichaguliwa watahakikisha uboreshwaji wa barabara na kujenga nyingine ili kuharakisha mawasiliano ya barabara ndani ya Mkoa wa Morogoro na kuunganisha na mikoa mengine.
Ameongeza kuwa miaka mitano ijayo ilani ya chama imeelekeza vijiji ambavyo havina umeme kufikiwa na umeme kulingana na mpango wa serikali ya CCM ambao hadi kufikiwa mwaka 2025 Tanzania yote inapata umeme.
Samia Suluhu Hassan amehutubia Wananchi wa Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro.