Chama Cha Mapinduzi (CCM) imetanagaza mchakato wa kupatikana kwa mgombea wa nafasi ya kiti cha Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akitangaza mchakato huo mbele ya waaandishi wa habari katika ofisi za chama hicho mjini Unguja, Katibu wa itikadi na uenezi wa Chama hicho Shaka Hamdu Shaka amesema hatua hiyo imekuja baada ya aliyekuwa Spika Job Ndugai kujiuzulu nafasi hiyo Januari 6,2022.
Shakah amesema katika kutekeleza matakwa ya kikatiba mchakato huo unatoa fursa kwa wanachama wa Chama hicho wenye sifa kujitokeza kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo iliyoachwa wazi.
Aidha amesema zoezi la uchukuaji wa fomu litafanyika kuanza Januari 10 hadi 15 mwaka 2022 kwenye ofisi za Chama hicho zilizopo Makao Makuu Dodoma, Ofisi ndogo ya CCM Lumumba na Kisiwandui Zanzibar.