CCM tanga yataka mazingira wezeshi kwa Watumishi

0
176

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Tanga, Rajabu Abdulrahman ameitaka Serikali kuendelea kutengeneza mazingira wezeshi ya Watumishi wake ili waishi karibu na vituo vyao vya kazi lengo likiwa ni kurahisisha utoaji huduma kwa Wananchi.

Ameyasema hayo wakati wa ziara yake wilayani Pangani, iliyokuwa na lengo la kukagua miradi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kutembelea shule shikizi ya Kitundauwa iliyopo kata ya Kirare ambapo amesema watafanya jitihada kukarabati jengo lililopo karibu na shule hiyo ili kumwezesha mwalimu kuishi karibu na kituo chake cha kazi.

Akiwa katika Kijiji cha Kigombe wilayani Muheza Wananchi walimweleza kuhusu changamoto ya kukosekana kwa maji, hali iliyomfanya Mwenyekiti huyo wa CCM wa mkoa wa Tanga kumtafuta Waziri wa Maji Jumaa Aweso ambaye ametolea ufafanuzi suala hilo kwa kusema wapo kwenye hatua za kumtafuta mkandarasi ili aweze kuanza ujenzi wa mradi wa maji kwenye eneo hilo.