CCM : Migogoro ya wakulima na wafugaji sasa basi

0
132

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo ametaka migogoro ya wakulima na wafugaji iwe mwisho mkoani Morogoro.

Chongolo amesema hayo mara baada ya kuwasili wilayani Gairo kuanza ziara ya siku tisa mkoani Morogoro.

Amesema haiwezekani makundi hayo mawili kuendelea kugombea ardhi huku viongozi wa ngazi za vijiji na kata wapo.

Katika ziara hiyo ya siku tisa mkoani Morogoro, Katibu Mkuu huyo wa CCM Taifa ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Sophia Mjema.