CCM kuomboleza kwa siku 21

0
219


Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza siku 21 za maombolezo, kufuatia kifo cha Mwenyekiti wa chama hicho Rais  Dkt John Magufuli.
 
Akizungumza na Waandishi wa habari jijini  Dodoma,  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, -Humphrey Polepole amesema  kuwa kufuatia msiba huo chama hicho kimesitisha shughuli zote za chama na bendera zitapeperushwa nusu mlingoti.
 
Amesema viongozi wakuu wa CCM wa Tanzania Bara na Zanzibar wamekubaliana Kamati Kuu ikutane siku ya Jumamosi jijini Dar es salaam kwa ajili ya kujadili mambo mbalimbali.
 
CCM imewaomba Wanachama wote wa chama hicho na watu wote wenye mapenzi mema na CCM pamoja na Watazania wote kusimama imara na kuendelea kutafakari mchango wa kihistoria wa Dkt Magufuli katika maendeleo ya Taifa.