CAG atambulishwa kwa Wenyeviti wa Kamati mbalimbali za Bunge

0
168

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania – Job Ndugai, leo amempokea ofisini kwake jijini Dodoma na kisha kumtambulisha Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),- Charles Kichere kwa Wenyeviti wa Kamati mbalimbali za Kudumu za Bunge.

CAG Kichere ametambulishwa kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Serikali za Mitaa, -Vedasto Ngombale, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali Nangenjwa Kaboyoka na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, -Mashimba Ndaki.