Byabato: Ruzuku ya Serikali imeshusha bei ya mafuta

0
152

Naibu Waziri wa Nishati Stephen Byabato amesema serikali imetenga fedha ili kutatua changamoto ya umeme katika mikoa ya Iringa na Njombe, na kuongeza kasi ya kusambaza umeme katika vijiji na vitongoji mbalimbali nchini.

Akizungumza na wananchi wa mkoa wa Iringa Byabayo amesema, wakandarasi wanaendelea na kazi katika maeneo mbalimbali kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya umeme.

Aidha, amesema serikali imetenga shilingi bilioni 8 kwa ajili ya maandalizi ya kazi za awali za kutekeleza mradi wa kufua umeme kwa kutumia maporomoko ya maji ya Ruhuji na Rumakali.