Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, Maharage Chande amesema wanatarajia kuanza kuzalisha umeme katika Bwawa la Julius Nyerere Juni 2024, baada ya kukamilika kwa zoezi la ujazaji maji baada ya mvua za masika mwaka huo.
Amesema hayo leo ikiwa ni saa chache kabla Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ajazindua zoezi la kuanza kujaza maji katika bwawa hilo lenye uwezo wa kuhifadhi maji lita bilioni 32 ambalo ujenzi wake umefilia asilimia 78.68.
Akizungumzia mradi huo amesema “una hatua zifuatazo, kwanza kuchimba njia ya mchepuko ambayo kesho tunaifungua maji yaanze kujaa, pili kujenga tuta lenyewe la kukusanyia maji, tatu kuchoronga njia ya kuyaporomosha maji ili yaende kwenye mashine, nne kujenga mashine zenyewe ambazo unatoka nje unazifunga, mashine hizo ziko tisa.”
Amesema mradi huo utaenda kufanya wawekezaji wengi kuja Tanzania kwa ajili ya hali ya umeme, uchumi wa Tanzania utaenda kukua, mijini na vijijini uzalishaji umeme utaongezeka, utafiti wa mafuta na gesi utaongezeka kwa sababu nishati ya umeme ipo ya kutosha.