BURIANI

0
217

Shughuli ya kuaga miili mitano ya wafanyakazi wa Shirika la Afya na Maendeleo Tanzania (MDH) waliofariki dunia katika ajali ya ndege iliyotokea Bukoba mkoani Kagera tarehe 6 mwezi huu inaendelea katika viwanja vya Karimjee mkoani Dar es Salaam.

Wafanyakazi hao watano ni miongoni mwa watu 19 waliofariki dunia baada ya ndege hiyo iliyokuwa ikisafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Bukoba kupata ajali katika ziwa Victoria.