Bunge lapitisha bajeti ya wizara ya nishati

0
132


Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha bajeti ya wizara ya Nishati kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023.

Wizara ya Nishati imeomba kupatiwa shilingi triloni 2.9 katika mwaka ujao wa fedha ili iweze kutekeleza majukumu yakei.

Bajeti hiyo iliwasilishwa bungeni jijini Dodoma hapo jana na Waziri wa Nishati January Makamba na kujadiliwa na wabunge mbalimbali.

Akijibu hoja za wabunge waliochangia bajeti hiyo Waziri Makamba amegusia mageuzi yanayoendelea ndani ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na kuongeza kuwa serikali itaendelea kuliwezesha shirika hilo iĺi liweze kutekeleza majukumu yake kikamilifu.

“Kwa upande wa TANESCO, Serikali italiwezesha na kulipa nafasi kuendelea na mageuzi yanayoendelea ya kuliimarisha shirika na kuliwezesha kutoa huduma bora zaidi kwa wateja wake, katika mwaka ujao wa fedha, Shirika linategemea kuanza utekelezaji wa mradi wa kubadilisha mita za LUKU kwa kuweka mita janja (smart meters) ili kuwezesha wateja kununua umeme utakaoingia moja kwa moja kwenye mita zao na hivyo kuondoa usumbufu kwa wateja na kuongeza mapato ya TANESCO.” amesema Waziri Makamba